TANGAZA NASI HAPA (ADVERTISE WITH US CONTACT 0757768555, 0717396699, 0785829399)

TANGAZA NASI HAPA (ADVERTISE WITH US CONTACT 0757768555, 0717396699, 0785829399).

ZINGATIA HAYA MARA UANZISHAPO BIASHARA UTAFANIKIWA

 UNACHOTAKIWA KUFANYA PALE UNAPOANZISHA
BIASHARA 

Image result for PICHA ZA PESA

Najua nazungumza na mabilionea wakubwa,
kama si mabilionea wa sasa, basi ni mabilionea
wa baadaye. Wewe ni bilionea, nakutamkia hili na
unatakiwa kuamini pasipo kujali kwamba kwenye
akaunti una shilingi elfu moja au chini ya hapo,
unachotakiwa kuamini kwamba wewe ni bilionea.
Inawezekana umeanzisha biashara yako, kitu cha
ajabu kabisa, fedha hazikai, kila ukipata leo,
kesho hazipo, ili kuendesha biashara yako
inakupasa kukopa sehemu, ni kweli ulipata faida,
ila kwa nini ukope? Kopa wakati ukitafuta mtaji,
ila kama umeshafanya biashara na faida ukapata,
kwa nini ukope? Kwa nini usitumie faida
uliyoipata kukuinua hapo ulipo?
Wengi wanakutana na hali hiyo, si wewe tu, hata
mimi nilishawahi kukutana nayo, na si sisi tu,
amini hata mabilionea wakubwa walishawahi
kukutana na hali hiyo. Hivi unajua ni mabilionea
wangapi waliwahi kufilisika? Unamjua Muitaliano
Enzo Ferrari? Alipata fedha, akafilisika, akagundua
alipofanya makosa, akatafuta tena, akazipata.
Wewe kama binadamu wengine, unaweza kupata
fedha na kufilisika, hapa siwazungumzii wakina
Bakhresa, Mengi na wengineo, nakuzungumzia
wewe mwenye biashara ndogo, nataka biashara
yako ikue, utoke hapo ulipo na usogee mbele
zaidi, ufanikiwe na siku moja uitwe bilionea
Omari, Selemani, John, Hamisi, Sara, Anna, Peter
au jina lolote ulilokuwa nalo.
Hizi ni baadhi ya njia ambazo zinaweza
kukusaidia kufikia ubilionea japokuwa una
biashara ndogo au kipato kidogo.
1. WEKA MALENGO: Kitu cha kwanza
unachotakiwa kufanya kama mfanyabiashara ni
kuweka malengo. Hebu chukua karatasi, andika
malengo yako na kuyafanyia kazi. Kumbuka wewe
ni bilionea, usiweke malengo ambayo unadhani
kwamba pia ua utayafikia, ukiyaandika hayo, jua
hautotoa nguvu kubwa kupambana ili uyafikie
malengo hayo. Kama una mtaji mdogo, weka
malengo makubwa ya kufanikiwa, unapoweka
malengo makubwa zaidi ya ulichonacho
kitakufanya ujitoe zaidi, uongeze juhudi ili kufikia
kile unachokiwazia.
Mfano wewe ni mfanyabiashara mdogo, ukaweka
lengo kwamba mpaka mwaka kesho lazima
uanzishe biashara ya kuuza mahindi mitaani.
Sawa, si vibaya lakini ulitakiwa kuweka malengo
ya biashara kubwa zaidi. Kwa fedha hizohizo
ulizokuwa nazo, unaweza kuanzisha biashara ya
mahindi, ukijiwekea hivyo, jua kwamba
unayachelewesha mafanikio yako. Ninataka
ujitume kwa nguvu zote, ukiweka yale malengo
makubwa, utajiona huwezi kufika lakini ndiyo
yatakayokufanya kupambana zaidi, hutolala,
utapambana usiku na mchana ila ukiweka lengo
dogo, utasema subiri upumzike kwani lengo hilo
litakuja hata kama hutojitoa, hivyo ili ufanikiwe,
jiwekee lengo kubwa na hakika utapiga hatua.
Mfano mzuri mimi. Sikuwa na fedha kipindi cha
nyuma, ishu ya kuanzisha magazeti ilihitaji
msingi mkubwa sana, ila sikutaka kukwepa lengo
langu la kufanya hivyo. Ningeweza kusema niuze
machungwa mitaani, kweli ningeuza, lakini kwa
nini niweke lengo dogo? Je ningejitoa zaidi? Ili
nijitoe, ili nifanye kazi usiku na mchana ilikuwa ni
lazima niweke lengo kubwa, nikaweka, nikajitoa
na kufanikiwa. Kama Shigongo, yule mtoto
masikini ameweza, vipi kuhusu wewe?
2. USIOGOPE KUFELI: Ndiyo! Kuna watu waoga
sana, wanaogopa kufanya biashara fulani kubwa
kwa kuwa wanaogopa kuanguka. Rafiki yangu,
kuanguka ni sehemu moja ya maisha, ili usonge
mbele ni lazima uanguke. Huwezi kujua
kuendesha baiskeli kama hujaanguka, ni lazima
uanguke ili ujue, iko hivyo.
Mtoto anapoanza kutembea, kuna kipindi
anaanguka, mbona yeye hakati tamaa na kusema
kwamba kuanzia leo hatembei tena kisa
ameanguka? Akianguka, hunyanyuka na kutembea
tena, akianguka anajaribu tena.
Wewe kama mfanyabiashara mdogo au mkubwa,
jifanye mtoto, usiogope kufeli, ili usonge mbele, ni
lazima ufeli, huwezi kuwa mshindi siku zote, kuna
kipindi unashindwa, ukishindwa, unakaa chini na
kuwaza umeshindwa wapi, unajipanga na kurudi
tena kwenye gemu.
Kama ningekuwa naogopa kufeli, nakwambia
ukweli kwamba nisingekuwa hapa, labda leo
ningekuwa mtaani tu nafanya biashara
ndogondogo, kuogopa kufeli kungenifanya niwe
kulekule nilipokuwa nyuma. Ili ujifunze, ili upige
hatua ni lazima ufeli, ukifeli, unajifunza na
kusonga mbele.
3. WEKA UMAKINI NA FEDHA ZAKO: Siku zote
nimekuwa nikiwaambia watu, si vizuri kutumia
kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya unachoingiza.
Mwingine ana biashara inaingiza elfu ishirini kwa
siku, ila anataka kufanya matumizi yasiyokuwa na
faida kwa kutumia elfu thelathini. Ndugu yangu!
Huwezi kuishi kwa maisha haya halafu ukaja
kufanikiwa. Unatakiwa kuwa makini na fedha
zako.
Mwingine anasema, nimepata faida nyingi, acha
nikale bata! Ndugu zangu, bata haziishi, kila siku
zinaongezeka, baa hazifungwi, umezikuta na
utaziacha, kumbi za starehe kila siku
zinafunguliwa mpya.
Ithamini pesa yako, hata kama ni shilingi hamsini,
ithamini. Unapokuwa na elfu moja, inayokamilisha
hela hiyo ni shilingi hamsini, kama ukiwa na 950,
huwezi kupata 1000 kama huna hamsini, kwa
hiyo kwenye maisha yako ya kibiashara, hata
shilingi 50 ni muhimu mno kwako.
Usiipuuzie fedha yoyote ile, panga matumizi yako
ya kawaida, si muhimu sana kunywa soda kama
huna sababu ya kufanya hivyo! Hakuna umuhimu
wa kula chipsi kuku kama hakuna umuhimu wa
kufanya hivyo! Kwani usipokula chipsi kuku
utakufa? Kama una kiasi kidogo cha fedha basi
hata matumizi ya fedha yako hakikisha yanakuwa
madogo na si makubwa zaidi ya kile ulichokipata.
4. JENGA URAFIKI NA WENYE FEDHA: Hapa
simaanishi kwamba wasiokuwa na fedha inabidi
watengwe, hapana! Ila unatakiwa kuwa makini, ni
vizuri kutengeneza marafiki wapya lakini inabidi
uwe makini. Kabla ya kuwa nilivyo niliwahi
kuwasikia watu wakisema unapoanza kufanikiwa
unabadilika, nilipinga lakini nikaja kuona
inawezekana.
Unapokuwa umefika hatua fulani, automatic
unaanza kutafuta watu ambao wanaweza
kukuvusha kutoka hapo ulipo, watu wenye uwezo
wa kukufanya kufanikiwa zaidi. Kumbuka shuleni
kwenu, ni wanafunzi wangapi waliokuwa na akili
walikuwa marafiki wao kwa wao? Kwani
hawakuwa marafiki zako pia, walikuwa marafiki
zako ila wenyewe wakawa beneti, ipo hivyo.
Unapopata fedha, unapofanikiwa, jaribu
kutengeneza ukaribu na watu waliofanikiwa,
usiwaache wale wengine, kuwa nao ila usiwe nao
beneti kupindukia, kama unaona mtu haeleweki,
hana hamasa ya kukufanya kufanikiwa, kwa nini
uwe naye beneti? Muache awe rafiki wa kupiga
naye stori dakika kumi na kuondoka.
Unapokuwa siriazi kutafuta fedha, huna budi
kuwatafuta waliofanikiwa, wakufundishe kwa nini
wapo hapo, walipitia nyanja zipi mpaka
kufanikiwa hivyo? Ni lazima ujifunze kupitia wao
na hakika utafanikiwa.
5. USICHANGANYE BIASHARA NA URAFIKI/
NDUGU: Ndiyo! Wengi tunafeli hapa. Tunapopata
nafasi ya kufanya biashara, wengi tunakosa
kufanikiwa kwa sababu tu tumechanganya urafiki
katika biashara. Biashara ndogo lakini bado
unataka kukopesha, tena kwa watu ambao huna
uhakika kama watakulipa.
Unapoanzisha biashara, wengi watakuja kukopa
na si kununua, hebu jiulize, wakati hujaanzisha
hiyo biashara, mbona hawakuwa wakienda
kukopa sehemu nyingine? Jua sisi binadamu tuna
makusudi, tunapomuona mtu ameanzisha
biashara, mara nyingi tunataka kumuangusha
chini ili tumcheke, tumdhihaki kwamba kiko wapi
sasa! Unatakiwa kuwa makini sana, huu si muda
wa kupeleka urafiki na undugu katika biashara.
Unapoanzisha biashara na ikatokea umemuajiri
ndugu yako, mwambie wazi kwamba upo kama
mfanyabiashara na si kama ndugu, anapofanya
makosa, mchukulie hatua kama unavyomchukulia
mtu baki, ukimuacha kwa kuogopa lawama,
huyohuyo baadaye atakuja kukucheka.
Unapoona una hamu ya kula chipsi, na wewe
unaifanya biashara hiyo ya chipsi, nunua chipsi
zako, si kwamba ni zako basi na wewe ule bure.
Najua ni ngumu kwa watu wengine lakini inabidi
ufanye hivyo ili kuifanya biashara yako isimame.
Leo unapouza chipsi na kula bure, amini kwamba
kesho utataka uongeze na chipsi yai, keshokutwa
chipsi samaki, sasa ukifanya hivyo, hutofanikiwa
kwa hiyo ni lazima hata wewe mwenyewe ujidai.
Sina mengi, ila tukutane muda mwingine kwa
makala nyingine ya ujasiriamali. Kumbuka, wewe
ni bilionea, fanya mambo kama bilionea.

BY Dr Magope

No comments

Powered by Blogger.