SARATANI NI NINI!!?
IJUE AFYA YAKO
Na Dk Dominista Aaron
Daktari bingwa,
Ocean Road Cancer Institute
Saratani ni nini?
• Saratani ni uvimbe unaojitokeza mahala
popote ktk mwili wa mwanadamu. Uvimbe
usiokuwa na maumivu yoyote mwanzoni.
• Uvimbe huo waweza kukua taratibu au
haraka ila hatimaye husambaa mwilini na
kisha husababisha maumivu na dalili
nyinginezo hatari kwa maisha ya mgonjwa
huyo asipotibiwa mapema!!!
Aina za saratani
Neno saratani = Mwavuli
• Ziko aina zaidi ya 100 za saratani
kuzingatia mahali ilipoanzia: Ngozi, titi,
koo la hewa/chakula, tumbo, utumbo,
kongosho, ini, mifupa, misuli, tezi, damu,
ubongo, macho, kizazi, shingi ya kizazi,
kibofu cha mkojo, mirija ya mkojo, nk, nk.
• Saratani zina majina yake ya kitaalam
kudhihirisha zilikoanzia…
Viashiria hatari kwa saratani
• Visivyozuilika: Jinsia, Umri, Uwezekano
wa kurithi (5%), mionzi ya jua/migodini, nk.
• Vinavyozuilika: Mazoea mabaya hususan
uvutaji sigara/pombe kali, Ulaji mbovu,
kutofanya mazoezi, kutojishughulisha/
unene uliokithiri, kutojali mazingira safi na
salama kazini na viwandani, madawa ya
sumu ya kuulia wadudu, nk, nk.
• ??? Vidonge/vipandikizi/sindano za majira
Viashiria…
• Vinavyozuilika:
- Mila na desturi hatari/mbovu: Ndoa/ngono
za utotoni, kujamiiana kwa njia zisizo za
asili
• Maambukizi ya baadhi ya virusi, bakteria,
fangasi, magonjwa mengineyo ya zinaa
• Kushuka kwa kinga ya mwili, madhaifu
Saratani : Dalili
• Hakuna dalili iliyo maalum kwa saratani
peke yake!!!
Ila kwa kuanzia:
• Ni uvimbe (1:10) au chembechembe
hatari zilizohakikishwa kitaalam kuwa ni
saratani.
Dalili…
• Dalili zingine zinatokana na hatua ya
ugonjwa na mahali ulipo: Kutokwa
majimaji/damu, haja kubwa yenye
damu/nyeusi, kikohozi cha muda mrefu,
mafindifindo, kushindwa kumeza,
kupumua, shida ya mkojo, kushindwa
kutembea/kuvunjika kiungo ghafla, nk,nk
• ??? Maumivu mwanzoni (Ni adimu)
Saratani: Uhakiki wake
• Saratani itakuwa ni saratani pale tu
inapohakikishwa kwa njia ya kutoa
kinyama au ute wa chechembe husika
na kupimwa katika maabara maalum
(pathology laboratory)!!!
• Vipimo vingi vya kimaabara au radiologia
vinaonyesha tu mabadiliko yenye
kuashiria uwezekano na siyo uhakika!!!
Saratani ya shingo ya kizazi
• Hali halisi nchini Tanzania- Ndiyo
inayoongoza (asilimia 40%) kati ya
saratani zote nchini.
-Ndio inayochangia vifo vingi zaidi kwa
wamama wenye umri mdogo (miaka 30 –
40).
Saratani ya shingo...
• Inaanza kama uvimbe katika mdomo wa
kizazi, kisha hupasuka na kutoka damu na
kuwa donda lisilopona...
• Sababu inayopelekea kupata saratani hii
ni maambukizi ya kirusi aina ya HPV
(99%) yanayopatikana zaidi kwa njia ya
kujamiiana.
Saratani ya shingo...
• Mwanamke yeyote mwenye kushiriki au
aliyeshawahi kushiriki tendo la ndoa na
kupata maambukizi ya HPV aweza kupata
saratani ya shingo ya kizazi (30%).
• Ngono katika umri mpevu (kabla ya miaka
20-22) ni hatari akipata maambukizi ya
HPV.
• Kushuka kwa kinga ya mwili – ukimwi,
maradhi ya kusendeka/sugu, uzee, nk.
Uhusiano kati ya cacx na
ukimwi
• Yote huambukizwa zaidi kwa njia ya
ngono (ni magonjwa ya zinaa)!
• Mgonjwa mwenye nayo yote husababisha
kinga ya mwili wake kushuka zaidi
• Mwenye ukimwi ana uwezekano mkubwa
zaidi kupata saratani ya shingo ya kizazi
• Tiba humletea shida zaidi mgonjwa huyo
• Hata baada ya tiba uwezekano wa kurudia
tena upo.
Dalili za saratani ya shingo...
• Hatua za mwanzo za ugonjwa HAKUNA
dalili zozote ila tayari kunakuwepo na
mabadiliko endapo atachunguzwa afya.
• Hatua zilizoendelea: Kutokwa damu baada
ya tendo, nje ya mzunguko wa hedhi,
majimaji machafu na hatimaye kutokwa
mikojo/haja kubwa kupitia ukeni
• Kusambaa sehemu nyingine mwlini na/au
figo kuharibika kabisa.
Kuwanusuru wamama
• Kujenga tabia ya kuchunguza afya ya
uzazi kabla na baada ya kubeba ujauzito
• Kutibu maambukizi hususan maradhi ya
ngono
• Kupata tiba sahihi mara tu inapogundulika
• Chanjo kwa mabinti wetu (9-13) na kwa
wengine wenye uwezo wa kuilipia (≤50).
Kupunguza/kuzuia uwezekano wa
kupata saratani
• JALI NA EPUKA viashiria hatari
vinavyozuilika(66% ya saratani zinazuilika)
• JENGA MAZOEA YA KUPIMA AFYA
YAKO MARA KWA MARA.
• Tafuta tiba mapema endapo tatizo
litagundulika.
• Pata chanjo kwa zile saratani zenye
chanjo hususan binti wadogo miaka 9-
13 ili kuzuia saratani ya shingo ya
kizazi baadaye.
Kupunguza/kuzuia uwezekano…
• Tumia matunda na mboga aina zote kwa
mchanganyiko: Karoti, vitunguu, saumu,
kunde. Nafaka zisizokobolewa: Dona. Ulaji
bora, epuka unene. Mazoezi ya mwili na
kujishughulisha kikamilifu kwa kazi.
• Usingizi wa kutosha na mapumziko ya
kiasi baada ya kazi za kutwa.
• Mahusiano mazuri na wengine –
amani/kicheko kwa faida yako binafsi!
Mlo bora na kamili
• Hupunguza uwezekano wa kupata saratani
• Hupunguza kasi ya kukua kwa saratani
• Huboresha kinga ya mwili
Vituo vipaswavyo kutoa huduma
Huduma za uchunguzi wa afya hutolewa:
- Hospitali za serikali
- Hospitali za mission na watu binafsi
- Family planning clinics
- Ocean Road Hospital
- CHANJO kwa sasa inapatikana hospitali
za binafsi ila mipango iko mbioni kuchanja
wasichana miaka 9-13
HITIMISHO
• Uboreshaji wa afya yako ni jukumu lako
wewe mwenyewe.
• Kitu kizuri huigwa: Wenzetu ktk nchi
zilizoendelea wanajali –wanapima afya zao;
hivyo saratani zao hugundulika mapema na
kutibiwa
• Wakati muafaka wa kuinusuru afya yako ni pale
unapofahamu na kuchukua hatua!!!
• Bora kinga kuliko tiba. Tujali sana afya zetu.
AFYA NI TUNU BORA
No comments