JWTZ, TPDF YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA NA MAFUNZO
Job Vacancies and Training Opportunities at The Tanzania People’s Defence Force (TPDF) ,JWTZ
The Tanzania People’s Defence Force (TPDF) is the armed forces of Tanzania. They were set up in September 1964, following a mutiny by the former colonial military force: the Tanganyika Rifles. From its inception, it was ingrained in the troops of the new TPDF that they were a people’s force under civilian control. Unlike some of its neighbors, Tanzania has never suffered a coup d’état or civil war. The TPDF was given a specific mission: to defend Tanzania and everything Tanzanian, especially the people and their political ideology. Tanzanian citizens are able to volunteer for military service from 15 years of age, and 18 years of age for compulsory military service upon graduation from secondary school. Conscript service obligation was 2 years as of 2004.
To Read More about Job Vacancies and Mode of Application
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.
Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo.
Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-
a. Daktari Bingwa wa Meno – Dental Surgeon
b. Daktari Bingwa – Specialist Neurasurgeon
c. Mkemia (Chemisist)
d. Mteknolojia Msaidizi (Maabara) – Assistant Laboratory Technician.
e. Tabibu msaidizi – Assistant Clinical officer.
f. Katibu wa Hospitali –
g. Msaidizi wa kumbukumbu. – Medical Records (Certificate)
h. Daktari – Medical Doctors.
j. Afisa Muuguzi – Registered Nursing Officer.
k. Fundi sanifu vifaa tiba – Bio Medical Engineer.
l. Tabibu – Clinical Assistant (Certificate).
m. Mteknolojia msaidizi – Laboratory Assistant (Certificate)
n. Mfamasia – Pharmacist (Degree)
o. Mtoa tiba kwa vitendo – Physiotherapist (Diploma)
p. Afisa Muuguzi msaidizi – Assistant Nursing officer
Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-
a. Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b. Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist
c. Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.
d. Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri
e. Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.
f. Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School
Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).
g. Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja
na kusajiliwa na Bodi.
h. Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia
Magendo.
Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika
Kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Mgulani Dar es Salaam tarehe 17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.
Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa
usafiri, chakula na malazi.
Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na
yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale
yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao.
No comments