WAALIMU WA MAZOEZI KWA VITENDO MBARONI KISA MAPENZI NA WANAFUNZI
Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika ambapo
amesema kuwa waalimu wa wanafunzi hao wamekiuka maadili ya ualimu na
kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia kama hizo
zinaleta kichefu chefu kwa jamii.
“Inabidi
wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini
shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na
badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita,”amesema Lugangika
Hata
hivyo, kwa upande wa Afisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Lushoto, Kassim
Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike
muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.
No comments