TANGAZA NASI HAPA (ADVERTISE WITH US CONTACT 0757768555, 0717396699, 0785829399)

TANGAZA NASI HAPA (ADVERTISE WITH US CONTACT 0757768555, 0717396699, 0785829399).

UHURU KENYATTA ANAONYESHA KUONGOZA BAADA YA KUHESABIWA 80% YA KURA

Rais anaemaliza mhula wake nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anasemekana anaongoza matokeo ya uchaguzi wa rais, baada ya kuhesabiwa takriban asili mia 80 ya kura. Kwa mujibu wa hesabu za hadi sasa za tume ya uchaguzi, rais Uhuru Kenyatta amejikingia asili mia 55 huku mpinzani wake Raila odinga akijipatia asili mia 44. Mgombea huyo wa muungano wa upande wa upinzani NASA, anashuku matokeo hayo. Katika mkutano na waandishi habari, Raila Odinga amesema hesabu hizo ni za "uwongo". Anasema hesabu zilizokusanywa na muungano wa NASA zinaoyesha wazi kwamba yeye ndie anaeongoza matokeo ya uchaguzi wa rais hadi sasa. Kwa mujibu wa polisi na maafisa wa tume ya uchaguzi zoezi la kupiga kura limepita salama. Hata hivyo hali bado inatisha. Muungano wa upinzani NASA unazungumzia kuhusu visa vya udanganyifu na vyeti vya uchaguzi vilivyojazwa mapema. Lawama kama hizo zimetolewa pia na chama tawala cha Jubelee. Ripoti za hivi punde zinasema polisi walifyetua gesi za kutoa machozi kuwatawanya wapinzani waliokuwa wakiimba katika mji wa magharibi wa Kisumu.

No comments

Powered by Blogger.