KENYATTA AMJIBU RAILA ODINGA BAADA YA KUTANGAZWA KUWA RAIS.
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume Huru ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC), Rais Mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa ujumbe wake kwa aliyekuwa mpinzani wake mkuu, Raila Odinga.
Ujumbe
wa Kenyatta kwa Raila umekuja wakati ambapo mwanasiasa huyo ameendelea
kushikilia msimamo wa kupinga matokeo yanayotangazwa na IEBC akidai kuwa
yalichakachuliwa na kwamba mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu ulidukuliwa.
Akitoa
hotuba yake baada ya kutangazwa rasmi kuwa mshindi, Kenyatta alimtaka
Raila afahamu kuwa bado anahitaji kushirikiana naye katika kazi na
kwamba hana uadui naye kwani wote lengo lao ni kujenga Taifa moja la
Kenya.
“Tutafanya
kazi pamoja, tutakua pamoja, tutaliendeleza hili taifa pamoja na tuko
hapa tayari kuendelea kufanya mazungumzo na midahalo pamoja ili tuweze
kujenga hili taifa letu pamoja,” alisema Kenyatta.
Aliongeza
kuwa katika kila mashindano lazima kuna watakaoshinda na wale
watakaoshindwa, hivyo anawapongeza walioshinda hata kutoka kambi ya
upinzani na kwa wale walioshindwa wataendelea kushirikiana pamoja bila
kujenga uadui.
IEBC
ilimtangaza Kenyatta kuwa mshindi wa kiti cha urais kwa muhula wa pili
akiwa na kura zaidi ya milioni nane (asilimia 54.27) dhidi ya Raila
aliyepata zaidi ya kura milioni sita (asilimia 44.7)
No comments